Friday, 15 February 2008

Karibu katika Blogu ya Kweli ni Nguvu

Karibu sana katika blogu hii. Hapa ni mahali ambapo maswala mbali mbali yanayohusu imani ya Kikristo pamoja na mambo mengine tunayokutana nayo katika maisha yetu ya kila siku yatakuwa yakizungumziwa.

Katika maswala ya Kikristo, mada mbali mbali zitagusiwa, zikiwemo zile zinazohesabika kama tata (controversial). Lengo ni kustawisha fikra za udadisi kulingana na Maandiko Matakatifu, ili kuweza kukua katika imani kama Mungu alivyokusudia.

Hapa kwenye blogu ya Kweli ni Nguvu tunaamini kuwa, katika ukweli kuna nguvu inayoweza kumweka mwanadamu huru.

Msomaji unakaribishwa kutoa mchango wako kuifanya blogu hii kuwa ya manufaa zaidi kwetu sote.

Karibu sana.