Friday, 12 October 2012

Tuishije na mahausigeli?


Kwa watu wanaoishi mijini, hususani wana ndoa ambao wamejaliwa kupata watoto, kuwa na wasichana wasaidizi wa nyumbani ni jambo la kawaida. Hata hivyo, ukizungumza na wengi wao, watakueleza kero au adha wanazofanyiwa na wasaidizi hao. Ukifuatilia kwa makini utagundua mara moja kuwa tabia za wasaidizi hao zinafanana ijapokuwa wametoka katika maeneo tofauti ya nchi - iwe Iringa, Dodoma, Mbeya, Kigoma, Singida, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Ruvuma, nk. Aidha, kumekuwa na taarifa ya baadhi ya wasaidizi hao kuwafanyia watoto wa waajiri wao vitendo viovu kama vile ngono, kuwapiga bila huruma, nk. Je, ni nini sababu ya wasichana hao kuwa na tabia za jinsi hiyo? Na wana ndoa wanaotegemea huduma za wasichana hao wafanyeje kukabiliana na hali hii, ukizingatia kuwa kuacha kabisa kupata huduma yao ni vigumu kutokana na mtindo wa maisha ya mijini ambako baba na mama wanatoka asubuhi kwenda kutafuta riziki na kurejea jioni / usiku?

No comments: